Quantcast
Channel: Rweyemamu info blog
Viewing all 7806 articles
Browse latest View live

WAANDISHI WA HABARI MAGAZETI YA MWANANCHI, NIPASHE NA HABARILEO WATWAA TUZO ZA ULUGURU AWARD 2013-2014 MOROGORO.

$
0
0


Mwandishi Mpigapicha wa gazeti la Mwananchi, Juma Mtanda kushoto Mwenyekiti wa Morogoro Press Club na Mwandishi Mtangazaji wa Nipashe na Redio One, Idda Mushi (katikati) na John Nditi wa Habarileo kulia wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutwaa tuzo bora za uandishi bora za Uluguru award 2013-2014 zilizoandaliwa na kituo cha Maendeleo na Utamaduni katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Mambo Club April 12 mwaka huu.PICHA ZOTE/MTANDA BLOG.

Idda Mushi akionyesha tuzo yake, kushoto ni mgeni rasmi Joel Bendera ambaye ni mkuu wa mkoa wa Morogoro.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Joel Bendera kushoto akimkabidhi tuzo mwandishi mpigapicha wa kampuni ya Mwananchi Communition Ltd Morogoro, Juma Mtanda baada ya kushinda tuzo ya Uluguru Award 2013-2014, lengo likiwa ni kuchochea uajibikaji kwa kufuata misingi ya utawala bora katika nyanja mbalimbali iliyoandaliwa na Kituo cha Maendeleo ya Utamaduni (Kimau) kutokana na mchango katika kuripoti baadhi ya habari za migogoro ya wakulima na wafugaji, mafuriko yaliyowakumba wananchi wa la kijiji cha Magole yaliyotokea hivi karibuni katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Mambo Club Morogoro.


John Nditi akionyesha tuzo yake baada ya kukabidhiwa na mkuu wa mkoa wa Morogoro kushoto.
Huyu ni Cosma Cheka naye alitwaa tuzo kwa upande wa bondia aliyetwaa mataji mawili ya mchezo huo.
Mkurugenzi wa matawi ya benki ya CRDB, Nelie  Ndosa akitwaa tuzo
Mwandishi wa habari gazeti la Mwananchi Lilian Lucas Kasenene kulia akina na Juma Mtanda baada ya kutunuziwa tuzo hiyo.
Safu ya viongozi wa CRDB, ikiongozwa na Mkurugenzi wa matawi ya benki ya CRDB, Nelie  Ndosa na mkurugenzi wa CRDB, Pendo Asay kushoto baada ya kutwaa tuzo ya taasisi bora ya kifedha ya mwaka 2014.
Mkurugenzi wa kituo cha Maendeleo na Utamaduni, Anthony Mhando kulia akimkabidhi tuzo mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera kufuatia tuzo ya kiongozi bora.
Mkurugenzi wa kituo cha Maendeleo na Utamaduni, Anthony Mhando 
Sehemu ya waalikwa wa hafla ya tuzo hizo

Mkurugenzi wa kituo cha Maendeleo na Utamaduni, Anthony Mhandokulia akifafanua jambo kwa Bendera kushoto na Mourice Massala (katikati) muda mfupi kabla ya kuanza hafla hiyo.





Mwandishi wa Jamboleo Peter Kimath (katikati) akiwa na mtangazaji wa kituo cha redio cha Planet FM Morogoro, Walda Makongwa kushoto na ndugu yao kulia wakati wa tuzo hizo.

 

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Joel Bendera akizungumza wakati wa hafla ya utoaji wa tuzo hizo, kushoto ni Mkurugenzi wa kituo cha Maendeleo na Utamaduni, Anthony Mhando.

Na Lilian Lucas, Morogoro.
Watu kadhaa akiwemo mwandishi wa Kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, Juma Mtanda ametunukiwa  tuzo ya heshima ya Uluguru Award ya mwaka 2013/14, kuhusu uandishi wa habari na upigaji picha za matukio mbalimbali yanayogusa jamii, mkoani Morogoro.

Tuzo hiyo imetolewa na Kituo cha Maendeleo ya Utamaduni cha mjini Morogoro (Kimau).

Akitangaza tuzo zilizotunukiwa kwa taasisi mbalimbali, Mkurugenzi wa kituo hicho, Morogoro Anthony Mhando, alisema lengo ni kuchochea uajibikaji kwa kufuata misingi ya utawala bora katika nyanja mbalimbali.

Mhando alizitaja nyanja hizo kuwa ni pamoja na uandishi wa habari zinazogusa jamii, ujasiriamali, uwekezaji, utawala bora, michezo na usanii.

Mhando aliwataja washindi wa tuzo hizo kuwa ni pamoja na mpigapicha wa gazeti la mwananchi mkoa wa Morogoro, Juma Mtanda aliyetwaa tuzo hizo kutokana na mchango katika kuripoti baadhi ya habari za migogoro ya wakulima na wafugaji, mafuriko yaliyowakumba wananchi wa la kijiji cha Magole yaliyotokea hivi karibuni.

Wengini waliotwaa tuzo ya uandishi wa habari ni Mwandishi Mtangazaji wa kituo cha televisheni cha ITV ambaye ni Mwenyekiti wa Morogoro Press Club, Idda Mushi, John Nditi kutoka TSN na Walda Magongwa wa kituo cha redio cha Planet FM.

Kwa upande wa viongozi utawala bora ni mbunge wa jimbo la Morogoro mjini Abdullaziz Abood,  mkuu wa mkoa wa Morogoro, Joel Bendera huku ngazi ya wajasiliamali, Bacho Sadik Bacho ambaye ni Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara wenye viwanda na kilimo (TCCIA) akitwaa tuzo hiyo. Alisema Mhando.

Kwa upande wa taasisi za kifedha CRDB yenyewe iliibuka na tuzo ya taasisi bora ya kifedha huku kampuni ya uwekezaji kiwanda cha kusindika tumbaku (TLTC) wakitwaa tuzo ya kampuni bora wakati kwa upande wa michezo, jina la Shomari Kapombe likiibuka katika soka, Cosmas Cheka ambaye ni mwanamasumbwi, Azack Sokas aliyetwaa tuzo kupitia mchezo wa kareti.

Viongozi wa michezo ni Zumo Makame, Awadh Komba na Paschol Kianga ambaye ni mwenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Morogoro (MRFA) kwa wasanii Miss Tanzania 2013 Happness Watimanya na Afande Sele anayejisghuhulisha na muziki wa kizazi kipya huku mkuu wa mkoa wa Morogoro akiwa mgeni rasmi katika haflas hiyo iliyofanyika ukumbi wa Mambo Club.

KURASA ZA MAGAZETI YA UDAKU NA MICHEZO LEO JUMATANO APRIL 16,2014

MAGAZETI YA LEO JUMATANO APRIL 16,2014

NAIBU MEYA ARUSHA APEWA KICHAPO NA MGAMBO

$
0
0


Msofe na Nanyaro
Naibu Meya wa Jiji la Arusha, Prosper Msofe (kushoto) ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Daraja Mbili kupitia CHADEMA na Diwani wa Kata ya Levolosi, Ephata Nanyaro nae kupitia Chadema, wakisubiri kupata matibabu baada ya kupata kipigo kutoka kwa mgambo wa Jiji la Arusha leo wakati wakiwatetea Wamachinga.Kwa mujibu wa Diwani Nanyaro, anasimulia kwamba leo asubuhi alipata taarifa kuwa mgambo wa Jiji wanawapiga wananchi wafanyabiashara ndogondogo na kupora mali zao maeneo ya Kata yake, ndipo akaelekea kukutana na Naibu Meya kujionea hali halisi. Anasema alipofika alijaribu kuwasihi mgambo hao kuwa sio utaratibu kuwapiga wananchi maana hata taratibu za ukamataji haziruhusu kupiga raia.

Nanyaro anasema wakiwa wanawashauri mgambo hao, ghafla walishangaa na yeye amezingirwa na kuanza kupigwa sambamba na Msofe huku mgambo hao wakiwaeleza Madiwani hao kuwa wamekuwa na kiherehere sana.
Naibu Meya anenaAkizungumza na Blog hii Mh. Naibu Meya Prosper Msoffe ameeleza kiini cha tatizo kuwa yeye kama kiongozi wa wananchi amekuwa akipokea malalamiko mengi ya wananchi kupigwa, wengine kuvunjwa miguu, mali kuporwa na mgambo, mali kifadhiwa depoti hadi kuoza. Hivyo akaamua kufika eneo la depoti leo kujionea hali halisi na kuzungumza na mgambo na wananchi, baada ya kufika eneo la tukio alianza kushambuliwa kwa virungu na mateke, huku wakisema wewe umekuwa kiherehere sana na mtetezi wa wananchi sasa tunakukomesha. 
Mh. Naibu Meya alishangazwa pia kuona kiongozi mwenzake Diwani wa Levolosi kufika pale nae akapigwa, na kuhoji kama yeye Naibu Meya amepigwa, hali ikoje kwa wananchi wa kawaida!??
Hatua za kisheria dhidi ya mgambo hao
Hadi tunaandika taarifa hii, Madiwani hao walikuwa wanaandaa utaratibu wa kushughulikia swala hilo wakidai kwamba mgambo hao wameonesha utovu mkubwa wa nidhamu na ukiukwaji wa sheria kwa kuwapiga waajiri wao.  Msofe na Nayaro wamelaani vikali tukio hilo na kuahidi kufuatilia ili sheria ichukue mkondo wake na iwe fundisho wa wengine.
2
Kadi ya matibabu ya Kituo cha Afya Levolosi, ikionyesha Mh. Naibu Meya ALIVYOUMIZWA
5 (2)
Wananchi na Wanachama wa Chadema Wakiwa nje ya Geti la depoti ya Jiji na Kituo cha Afya cha Levolosi wakisubiri hatma ya Viongozi wao.
4
1b
Diwani Nanyaro na Naibu Meya Msofe wakimweleza Mwandishi Filbert Rweyemamu hali ilivyokuwa hadi kupigwa kwa kile walichodai kutetea wananchi wanyonge dhidi ya uonevu, ukatili na ukandamizaji unaofanywa na askari wa Jiji.
11
‘Siamini kama Wafanyakazi wangu wanaweza nishambulia kiasi hiki’ Maneno ya Nanyaro akikagua ripoti ya dakatari
IMGP1057
Mh Kessy,  Diwani wa Kaloleni (anayeongea na simu) alipofika Hospitalini hapo kuwajulia hali viongozi wenzake.

PRIZE-GIVING CEREMONY FOR THE ‘BACK TO SCHOOL’ ESSAY COMPETITION WINNERS

$
0
0

In January 2014, Shule Direct organized an essay competition for Secondary School students titled ‘Back to School’. Students, Form II – Form IV, were required to write on the most interesting topic they had learnt at school, why they think it was interesting and how they can use the knowledge from the topic to help the community.

It was open from 24th of January up until 24th March 2014. Over 200 entries were submitted, out of which 186 qualified for the first round of the judging process. Among the 186 qualified essays, 103 were boys and 83 were girls. 27 Secondary Schools from 7 regions participated in the competition. The schools with the most entries were School of St. Jude of Arusha, Loyola High School of Dar, Azania Secondary School of Dar, Zanaki Secondary School of Dar and Morogoro International School of Morogoro.

The 1st place winner, Kazim Mohamed of Al- Muntazir Islamic Seminary, gets 500,000/- in cash, a Samsung tablet and three textbooks. 2nd place winner, Joseph Muhweza of School of St. Jude of Arusha gets 400,000/- in cash, a Samsung tablet and three textbooks. 3rd place winner, Rogate Exaudi Maro of Loyola High School gets 300,000/- in cash, a Samsung tablet and three textbooks. 4th place Achile Tigawa of Azania Boys Secondary School gets 200,000/- in cash and three textbooks. 5th place, Zawadi Issa Silim of Zanaki Girls Secondary School gets 100,000/- and three textbooks. The Semi- finalists (Top 25) are each awarded a set of three textbooks.

Shule Direct organized the competition to highlight the value of education for students in Secondary Schools, to cultivate academic competitiveness and academic excellence among students, to enable students to relate academic solutions to real-life challenges, to promote communication skills and confidence, to give a platform for young people to participate and share their opinions and to appreciate and recognize efforts by hardworking students.

Back to School Essay Competition 2014 was sponsored by Vodacom Tanzania as the main sponsor and other sponsors are Samsung, Radar Education, UNESCO Tanzania and Bongo5. It is an annual competition scheduled to take place at the beginning of the academic year for all Secondary School students in Tanzania.
1st Place Winner Kazim Mohamed Receives his Prize.
2nd Place Joseph from St. Jude.
3rd Place Winner Rogate Maro.








KURASA ZA MAGAZETI YA UDAKU NA MICHEZO LEO ALHAMIS APRIL 17,2014

SOMA MAGAZETI YA LEO ALHAMISI APRIL 17,2014

UKAWA WASUSIA BUNGE MAALUM LA KATIBA

$
0
0

Mjumbe wa Bunge Maalumu la Katiba, Prof Ibrahimu Lipumba akizungumza katika kikao cha bunge jana ambapo alitangaza kujitoa kwa baadhi ya wajumbe kuendea na mchakato wa kupitisha Rasimu ya Katiba, mjini Dodoma jana. Picha na Edwin Mjwahuzi 

Dodoma. Mambo yamebadilika. Ukimya ulitawala jana katika Ukumbi wa Bunge mjini Dodoma, baada ya wabunge zaidi ya 200 ambao ni wanachama wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kususia vikao vya Bunge hilo.
Ilikuwa ni saa 10:31 jioni baada ya Mjumbe wa Bunge hilo ambaye pia ni Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba alipohitimisha uchangiaji wake akisema: “Ukawa hatuwezi kuendelea kushiriki dhuluma dhidi ya wananchi kwa kupitisha Katiba ambayo ni kinyume cha matakwa yao.”
Baada ya kauli hiyo aliondoka akifuatiwa na Mwenyekiti wa Ukawa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia na wajumbe wao kutoka nje ya Bunge.
Ukimya ulitawala

takriban dakika mbili hivi na baada ya wajumbe hao kutoka, Makamu Mwenyekiti wa Bunge Maalumu, Samia Suluhu Hassan aliwaelekeza makatibu kuhesabu wajumbe ili kuona kama akidi imetimia ili waendelee na kikao.
Baadaye aliliambia Bunge kuwa makatibu wamemweleza hawahitaji akidi kwa kuwa kikao kilikuwa kinaendelea wakati Ukawa walipotoka nje ya ukumbi.
Hotuba ya Lipumba
Profesa Lipumba alianza kwa kunukuu Gazeti la Mwananchi la Aprili 14, mwaka huu katika sehemu inayosema; “Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Uratibu na Bunge) ameanza kampeni kanisani kwa kuwataka wananchi kupinga serikali tatu zilizopendekezwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, vinginevyo nchi itatawaliwa na jeshi kwa kuwa serikali ya muungano itashindwa kuwalipa mishahara wanajeshi.”
Alisema yeye ni muumini wa dini ya Mwenyezi Mungu lakini anaafiki mapendekezo yaliyoletwa bungeni hapo na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoundwa na Rais.
“Hii ni kauli ya Waziri Lukuvi ndani ya Kanisa la Methodist wakati wa sherehe ya kumsimika Mchungaji Joseph Bundala kuwa Askofu na Waziri Lukuvi alikuwa anamwakilisha Waziri Mkuu.”
Alisema inasikitisha kwa sababu kauli hiyo inafanana na ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa wakati akihutubia Bunge Maalumu.
Alisema kauli za Lukuvi zinatisha baada ya kusema Wazanzibari ambao wanataka kuwa na nchi yao hawawezi kujitegemea, bali wanataka wapate nafasi ya kujitangazia kuwa ni nchi ya Kiislamu.
“Waziri anaweza kusema hivyo ndani ya kanisa? Kawahamasisha mpaka yule kiongozi wa kanisa akasema ili kudumisha Muungano bora Katiba ya Zanzibar ifutwe ili iwepo moja ya nchi moja ambayo inadumisha Muungano,” alisema.
Alisema Lukuvi alikuwa akiwaaminisha kuwa mfumo wa serikali tatu ukipita kutakuwa na mapinduzi na nchi haitatawalika na hivyo watu watashindwa kwenda kusali makanisani.
“Kama ndugu zetu wa Zanzibar wangekuwa wanahitaji serikali moja tungekuwa na utaratibu mzuri tu, lakini siyo wanachama wa CUF, siyo wa CCM, Wazanzibari wote hawataki muungano wa serikali moja,” alisema.
Alisema Tume ya Mabadiliko ya Katiba imetoa mapendekezo ya serikali tatu kutokana na ukweli huo. “Hoja zilizoletwa hapa ni hoja za serikali moja, si hoja za serikali mbili lakini wenzetu moja hawataki, kwa hiyo tunahitaji Muungano ambao tutakuwa na maridhiano ya pande zote mbili,”
“Wengi wamenukuu makala niliyoitoa katika kituo cha TCD (Kituo cha Demokrasia Tanzania), ambayo iliunda Baraza la Katiba na mimi nilichambua mapendekezo ya Tume nikasema kwa mapendekezo yaliyomo ndani ya Rasimu ya Katiba hayatakidhi mapato ya shirikisho.”
Alisema wajumbe wanaomnukuu wanaishia hapo bila kwenda katika mapendekezo aliyoyatoa.
“Wamenisifu sana ni mchumi mahiri, basi waendeleze sifa hizo kwa mapendekezo niliyoyatoa ya mapato ya kukidhi uendeshaji wa serikali ya shirikisho.
“Nimeeleza katika hali halisi kuwa utaratibu mzuri ni mapato ya kila serikali kuchangia katika shirikisho na mambo haya yaandikwe katika Katiba. Katiba inaweza ikasema wazi asilimia 20 ya mapato yote yanayokusanywa Zanzibar au Tanganyika yataenda kwenye shirikisho.”
Alitaka pia kuwekwa kwa misingi mizuri ya kukusanya kodi na kutumia fedha za wananchi ndani ya katiba ya muungano ambayo ndiyo katiba mama.
“Lakini ndugu zangu mjadala wetu unavyokwenda utadhani kuwa Rasimu ya Katiba iliyoletwa imeletwa na CUF au na Chadema au na NCCR-Mageuzi, au Wapemba,” alisema.
Alisema ukurasa wa kwanza wa Rasimu ya Katiba unaeleza kuwa toleo hili la Rasimu ya Katiba lilichapishwa katika Gazeti la Serikali kwa mujibu wa Kifungu cha 20(2) ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Sura ya 83.
Alisema hiyo ni rasimu ya Tume ya Rais na si rasimu ya Wapemba.
Hata hivyo, alisema mjadala unaoendelea bungeni umekuwa na utaratibu wa ubaguzi... “Watu wamebaguliwa humu na viongozi wakubwa wanapiga makofi, Bunge hili limekuwa kama Bunge la Intarahamwe. Hii ni hatari kwa nchi yetu. Wapemba, Waarabu, Wahindi, Wakongo,” alisema.
“Hii hatuhitaji, tunahitaji katiba ambayo itahakikisha kila mwananchi anapata haki yake wote tuwe sawa bila kujali rangi zetu, jinsia zetu, makabila yetu, huu ndiyo msingi aliotuachia Mwalimu Nyerere tuenzi msingi huo.”
Alilalamikia kile alichokiita kuwa ni ubaguzi ndani ya Bunge na kwamba kama Serikali haikutaka Katiba Mpya kwa nini imepeleka wabunge Dodoma? Pia alihoji ni kwa nini ilitumia Sh70 bilioni katika Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
“Kwa nini mmetufikisha hapa? Jengo hili nimeambiwa limekarabatiwa kwa Sh8.2 bilioni hali hamuamini Rasimu ya Katiba ama ilikuwa ni utaratibu wa kupata hizo asilimia 10, ndiyo maana mmekarabati kwa gharama kubwa?” alisema.
“Tunataka CAG (Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali), akague matumizi ya fedha zilizotumika. Utatumiaje fedha nyingi wakati hiyo katiba iliyowasilishwa kumbe huitaki kabisa.
“Hakuna utaratibu wowote wa kupiga kura na kufanya maamuzi kuhusu sura hizi mbili. Tumechoka kusikiliza matusi. Tumechoka kudharau mawazo ya wananchi, tumechoka ubaguzi, hatuwezi kuwa sehemu ya kundi linalohamasisha ubaguzi ndani ya Tanzania hili hatukubali,” alisema.

BARABARA YA KONGOWE – MJI MWEMA – KIGAMBONI TAYARI INAPITIKA

$
0
0

Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) kwa kushirikiana na Jeshi la Wananchi la Tanzania wamefanikisha kuifungua barabara ya Kongowe kuelekea Mjimwema hadi Kigamboni ambayo ilijifunga kutokana na kukatika kwa kalvati katika mto Mtokozi . Kalvati hilo lilibomolewa na mvua kubwa zilizonyesha kwa siku kadhaa hapa jijini.

Hapo jana siku ya Jumanne, Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli pia alishirikiana na watendaji kwa siku nzima akiwa eneo la Mpiji kuhakikisha barabara ya Dar es Salaam kuelekea Bagamoyo inaanza kupitika tena baada ya kuwa imejifunga kwa takriban siku tatu. Sehemu hii ya barabara iliathiriwa na mafuriko yaliyotokana na mvua kubwa zilizonyesha katika kipindi cha hivi karibuni. Matengenezo katika daraja la Mpiji yalikamilika jana usiku na magari yameanza kupiti bila ya matatizo.

Siku ya Jumatatu daraja jingine katika katika mto Kizinga kwenye barabara ya Kilwa eneo la Mbagala Kongowe ilifunguka baada ya kazi ya usiku kucha iliyoongwozwa na Waziri Magufuli kufanikisha kukamilisha matengenezo katika sehemu hiyo yenye magari mengi. Barabara ya Kilwa ndiyo kiungo kikuu cha usafiri wa barabara kati ya Dar es Salaam na mikoa ya kusini.

Aidha katika siku hiyo hiyo ya Jumatatu, daraja la Ruvu pia lilianza kupitisha bagari baada ya sehemu ya barabara iliyokuwa imeharibika kutokana na mafuriko, kukarabatiwa.
Matengenezo yakiendelea katika Daraja la Mpiji.
Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akifuatilia matengenezo katika Daraja la Mpiji.
Waziri Magufuli akijionea madhara ya mafuriko katika barabara ya Kilwa eneo la mto Mzinga eneo la Mbagala Kongowe.
Waziri Magufuli akiwa kazini usiku katika eneo la mto Kizinga.
Hali ilivyo sasa katika eneo la Mto Kizinga kwa sasa.
Hali ilivyokuwa katika daraja la Mto Mtokozi katika barabara ya Kongowe - Mjimwema - Kigamboni.
Hali ilivyo sasa katika barabara ya Kongowe - Mjimwema - Kigamboni.

MAGAZETI YA LEO IJUMAA APRIL 18,2014

KURASA ZA MAGAZETI YA UDAKU NA MICHEZO LEO IJUMAA APRIL 18,2014

RAIS JAKAYA KIKWETE AKABIDHIWA RASMI TUZO YA KIONGOZI BORA BARANI AFRIKA KUTOKA KWA WAZIRI WA MAMBO YA NJE IKULU JIJINI DAR ES SALAAM..

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) akipokea Tuzo ya Utumishi Bora wa Umma Barani Afrika kutoka kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Benard Membe (kulia) kufuatia mchango mkubwa alioutoa kwa maendeleo ya wananchi wa Tanzania na Bara la Afrika.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) akisoma ujumbe ulioandikwa kwenye Tuzo ya Utumishi Bora wa Umma Barani Afrika aliyokabidhiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Benard Membe (kulia) leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Benard Membe (kulia) akisoma ujumbe ulioandikwa kwenye cheti kilichoambatana na Tuzo ya Utumishi Bora wa Umma Barani Afrika aliyokabidhiwa Rais Jakaya Kikwete leo Ikulu jijini Dar es salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Benard Membe (kulia) akimkabidhi  Rais Jakaya Kikwete (kushoto) cheti kilichoambatana na Tuzo ya Utumishi Bora wa Umma Barani Afrika  leo Ikulu jijini Dar es salaam.
 
Na Aron Msigwa- MAELEZO.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo Ikulu jijini Dar es salaam amepokea Tuzo ya Utumishi Bora wa Umma Barani Afrika kufuatia mchango mkubwa alioutoa  kwa maendeleo ya wananchi wa Tanzania na Bara la Afrika.
 
Akiwa mwenye furaha mara baada ya kupokea tuzo hiyo ambayo awali ilipokelewa kwa niaba yake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe jijini Washngton Marekani,  Rais Kikwete amesema kuwa ameipokea tuzo hiyo kwa moyo wa shukrani na heshima kubwa kufuatia imani kubwa iliyoonyeshwa kwake na kwa watanzania.
 
“Nimeipokea tuzo hii kwa moyo wa ukunjufu, ni tuzo ya watanzania wote kwa sababu mambo yote niliyoyafanya sikuwa peke yangu nimeyafanya kwa kushirikiana na watanzania wote” Amesema Rais Kikwete.
 
Rais Kikwete amesema kuwa amepokea tuzo hiyo kufuatia wasomaji na wadau wa Jarida la African Leadership Magazine ambalo huchapishwa mjini London, Uingereza na mjini Washington kuonyesha imani juu yake kwa kumchagua kwa njia ya kura ya maoni kama kiongozi aliyetoa mchango mkubwa zaidi kwa maendeleo ya wananchi wake katika Bara la Afrika kwa mwaka 2013.
 
“Nawashukuru sana African Leadership Magazine, kwangu ni heshima kubwa nawaomba watanzania tuendelee kushirikiana wenzetu duniani wanaona, wanatambua na kuthamini mchango wetu” Amesisitiza Rais Kikwete.
 
Awali kabla ya kumkabidhi Rais Jakaya Kikwete Tuzo hiyo na cheti cha shukrani Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Benard Membe amesema kuwa tuzo hiyo ni heshima kwa taifa la Tanzania kufuatia juhudi kubwa alizoonyesha Rais Jakaya Kikwete katika kuboresha maisha ya watanzanzania.
 
Amesema  kuwa wasomaji na wadau wa jarida maarufu la kimataifa la African Leadership Magazine wamemuona Rais Kikwete kuwa Kiongozi Bora wa Afrika aliyetoa mchango mkubwa zaidi katika maendeleo ya kiuchumi ya wananchi wake kwa mwaka 2013 kwa kumpigia kura nyingi za maoni.
 
Aidha ameeleza kuwa Rais Kikwete alitangazwa kuwa mshindi wa tuzo hiyo katika sherehe kubwa iliyotangazwa na kuonyeshwa moja kwa moja na mitandao mbali mbali ya kijamii duniani pia kuhudhuriwa na watu mbali mbali mashuhuri wakiwemo mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Marekani na Naibu Spika wa Bunge la Tanzania Mheshimiwa Job Ndugay ambaye alikuwa Washington kikazi.
 
Wengine ni Mwakilishi katika Bunge la Wawakilishi wa Jimbo la Georgia nchini Marekani na mwenyekiti wa wabunge weusi katika Bunge hilo, Bi. Dee Dawkins-Haigler na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mheshimiwa Liberata Mulamula.
 
Rais Kikwete amepata tuzo hiyo akimfuatia Rais wa Sierra Leone , Mheshimiwa Ernest Bai Koroma, ambaye alishinda Tuzo hiyo mwaka 2012.

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI APRIL 19,2014

AZAM FC YAKABIDHIWA KOMBE LA UBINGWA WA VODACOM LEO,YANGA NA SIMBA ZAGAWANA POINTI

$
0
0

 Wachezaji wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Azam FC ya Chamazi Dar es Salaam wakishangilia baada ya kuweka historia ya kutwaa Ubingwa wa Soka Tanzania 2013-2014. Ubingwa huo ulikuwa unashikiliwa na Yanga iliyoambulia nafasi ya pili na leo ikitoka sare na Simba 1-1.
Mshambuliaji wa timu ya Yanga , Hamis Kiiza (kulia) akiwania mpira na beki wa timu ya Simba, Nassor Masoud, katika mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam leo.hadi mwisho wa mchezo,matokeni Yanga 1-1 Simba.
Mshamuliaji wa pembeni wa timu ya Yanga,Simon Msumva (kulia) akijaribu kuwatoka mabeki wa timu ya Simba, katika mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam leo.hadi mwisho wa mchezo,matokeni Yanga 1-1 Simba.
Mshambuliaji wa timu ya Yanga Didier Kavumbagu (katikati) akiwatoka mabeki wa timu ya Simba katika mchezo wa Ligi kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam leo.hadi mwisho wa mchezo,matokeni Yanga 1-1 Simba.
Wachezaji wa timu ya Yanga,wakishangilia goli lao la kusawazisha.

AZAM FC WATAWAZWA RASMI KUWA MABINGWA WA LIGI KUU YA BARA

$
0
0


Bryan Umonyi wa Azam FC akifunga bao la pekee katika mchezo wao dhidi ya Ruvu JKT katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi, jijini Dar es salaam. 
Bryan Umonyi wa Azam FC akifurahia kufunga bao la pekee katika mchezo wao dhidi ya Ruvu JKT katika uwanja wa Azam Complex, Chamazi, jijini Dar es salaam. 
Wachezaji wa Azama wakifurahia bao hilo
Furaha ya ushindi
Mashabiki
Rais wa TFF Jamal Malinzi akiwa na viongozi wa Azam FC jukwaa kuu
 Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) akimkabidhi Kombe la ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Nahodha wa Azam FC, John Bocco jioni hii baada ya kuifunga bao 1-0 JKT Ruvu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Mabingwa wakisherehekea na taji lao, sherehe za ubingwa zimeendelea Azma Complex hadi usiku wa manane. 




KURASA ZA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI YA PASAKA APRIL 20,2014

ASKOFU KKKT IRINGA DR MDEGELA ATAKA UKAWA WASIRUHUSIWE KUENEZA CHUKI ,ATAKA WAREJEE BUNGENI AMA WAFUNGASHE VIRAGO WARUDI NYUMBANI ASEMA SERIKALI NI MBILI PEKEE

$
0
0

Askofu Mkuu wa Kanisa la Kilutheri (KKT) dayosisi ya  Iringa  Dr.OwdenburgMdegela
Wachungaji na  msaidizi wa Askofu kulia wakifuatilia salam za  pasaka zilizokuwa  zikitolewa na askofu Dr Mdegela
waumini  wa KKKT usharika wa kanisa  kuu leo

Waumini wa kanisa  hilo na  wageni kutoka nje wakifuatilia salama za askofu Dr Mdegela


MAGAZETI YA LEO APRIL 21,2014

MAGAZETI YA UDAKU LEO JUMATATU APRIL 21,2014

MAGAZETI YA MICHEZO NA BURUDANI LEO APRIL 21,2014

Viewing all 7806 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>