Quantcast
Channel: Rweyemamu info blog
Viewing all 7753 articles
Browse latest View live

KINANA NA UJUMBE WAKE WAWASILI ZANZIBAR KUZINDUA KAMPENI ZA CCM LEO

$
0
0



Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (watano kulia) na ujumbe wake wa viongozi waandamizi kutoka makao makuu ya CCM, wakiwa kwenye chumba cha nahodha walipokuwa wakisafiri kwa boti ya mwendokasi kutoka Dar es Salaam, kwenda Zanzibar kwa ajili ya kushiriki uzinduzi wa kampeni za CCM, uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Dimani, leo. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo

Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akihoji moja ya kifaa cha kuongozea boti ya mwendo kasi kinavyofanya kazi.

Karibu Zanzibar

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Rodrick Mpogolo akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mjini Magharibi, Aziza Mapuri baada ya msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kuwasili Bandari ya Zanzibar leo
"NAAM TUMEWASILI KWA MUDA SAHIHI" Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimwambia Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Zanzibar Vuai Ali Vuai baada ya kuwasili Bandari ya Zanzibar leo
Katibu Mwenezi wa CCM, Humphrey Polepole (kushoto) baada ya kuwasili Bandari ya Zanzibar
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo (kushoto) alipowasili Bandari ya Zanzibar leo

Humphrey Polepole akilakiwa baada ya msafara wa Kinana kuwasili Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui leo
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mjini Magharibi Aziza Mapiri akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kuhusu hali ya kampeni za uchaguzi mdogo wa Ubunge jimbo la Dimani walipokuwa katika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar leo


Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na msafara wake wakitazama eneo alilouliwa muasisi wa Mapinduzi ya zanzibar, Hayati Abeid Amani Karume katika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar, leo





Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiagwa na viongozi wakati akitoka Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Zanzibar kwenda kwenye mapumziko kabla ya kwenda kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Dimani leo jioni. Picha zote na Bashir Nkoromo

MAMILIONI YA KUZIMA MWENGE SIMIYU YA JENGA SHULE YA WATOTO WA WAFUGAJI MALINYI

$
0
0

Na Humphrey Shao,Globu ya Jamii Malinyi.

Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi ni moja ya Wilaya mpya hapa nchini zilizoundwa kutokana na ukubwa wa mkoa wa Morogoro kwa lengo la kuzidi kuongeza huduma za kiserikali kwa wananchi walio pembezoni hili kupunguza gharama za wananchi kutembea umbali mrefu.

Malinyi ambayo imezaliwa kutoka katika Wilaya Mama ya Halamashauri ya Wilaya ya Ulanga ambayo ilionekana kubwa kuliko kawaida na kushindwa kukidhi kuwahudumia wakazi wa malinyi kutokana na umbali wa kijiografia.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Malinyi ,Marcelin Ndimbwa, akikagua ujenzi wa madarasa ambayo yamejengwa kwa ajli ya watoto wa wafugaji Rumbanga.

Marceline Ndimbwa ni Mkurugenzi wa kwanza katika halmashauri hiyo mpya kuteuliwa na Rais wa awamu ya tano Daktari John Pombe Magufuli ili kuhakikisha maendeleo ya wilaya hiyo yanafanana na sehemu nyingine.

Ndimbwa amekuwa ni mkurugenzi wa halamashauri hiyo huku akikabiliana na changamoto kubwa ya mgogoro wa ardhi baina ya wakulima na wafugaji na changamoto ya miundombinu ya elimu katika jamii kubwa ya wafugaji.

Ndimbwa anasema kuwa Rumbanga ni moja ya maeneo ambayo hayapo mbali na mji wa Malinyi lakini yamekuwa na jamii kubwa ya wafugaji wa kabila la kisukuma huku wakiwa na changamoto ya kutokuwa na shule ya msingi, Sekondari na huduma za afya.

Ndimbwa anasema kuwa mbali na changamoto zote hizo lakini ameamua kuanza na changamoto kubwa ya kutokuwepo na shule ya msingi katika eneo hilo la Rumbanga.

“kiukweli hali sio nzuri katika eneo la Rumbanga kwani shule iliyopo ni ya nyasi ambayo imejengwa na wanakijiji wenyewe na aina walimu wa kufundisha zaidi vijana wawili ambao wamemaliza kidato cha nne na kuamua kujitolea katika kuwafundisha wadogo zao ambao wapo kuanzia darasa la kwanza mpaka la nne”amesema Ndimbwa.

 Ndimbwa anasema kuwa mara baada ya kuona mazingira hayo wakaona ni ulazima wa kuamua kujenga shule hiyo kuwa ya kisasa kutokana changamoto ya umbali kufata shule ambayo ipo kilometa 34 kutoka hapo Rumbanga na wanafunzi hao kutakiwa kutembea kwenda na kurudi katika shule ya msingi Mwembeni hali iliyochangia watoto wengi kuacha masomo na watoto wa kike kupata ujauzito katikati ya masomo na kulazimika kuacha shule.

Anataja kuwa katika hatua za awali zilizochukuliwa na halmashauri yake katika kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi na  sera ya Rais Magufuli ya kupata elimu bure na sio bure tu bali iliyobora kwa wanafunzi, Serikali ya Wilaya imeamua kubuni arambee kutoka kwa jamii ya wafugaji na kutenga fedha kadhaa kwa ajili ya kujenga majengo ya kisasa ya shule ya msingi Rumbanga ambayo imeanza kutokana na jitahada za watu wa jamii hiyo ya wafugaji.

“hatua ya kwanza niliyochukua ni kuchukua fedha za zilizotengwa kwa ajili ya kwenda Simiyu kuzima mwenge kiasi cha shilingi milioni 4 zipelekwe Rumbanga kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo hivyo kuongeza hali ya mwamko kwa wakazi wa kijiji hicho chenye jamii ya wafugaji” anasema Ndimbwa.

Ndimbwa anasema wanafunzi hawa pindi shule zitakapofungua awatasoma tena katika mabanda ya nyumba za nyansi kama ilivyokuwa awali hivyo watakingi katika madarasa ya kisasa kama ilivyo kwa watoto wengine wa Tanzania.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Malinyi, Nasoro Liguguda amesema kuwa uamuzi huo wa mkurugenzi wa mtendaji wa halmashauri umekuja wakati muafaka kwani jamii kubwa ya watoto wa wafugaji walikuwa wakiteseka kwa kupata elimu bora kutokana na wao kupendelea kuishi pembezoni na kuanzisha miji mipya.

Anasema wafugaji hao ambao kwa sasa wameamua kuishi malinyi hapo ni vyema nao wakapata stahiki zao za huduma za jamii kama ilivyo kwa jamii ya wakulima hili kupunguza migogoro.

Nae katibu wa kamati ya ujenzi wa shule hiyo, Joseph Paschal wanashukuru halmashauri kwa kuweza kuwapatia fedha za kujenga shule hiyo ambayo ni tumaini jipya kwa wakazi wa Rumbanga .

Anataja kuwa wakazi wa kijiji hicho walikuwa wakikumbwa na chngamoto nyingi wakati wa masika pindi wanapohitaji kwenda shule kutokana na kushindwa kuvuka mto Rumbanga ambao mara zote uwa unajaa maji hivyo kukusa masomo kwa kipindi chote.

Kwa upande wake mkurugenzi Ndimbwa amesema kuwa serikali imekwisha ridhia kuiweka shule hiyo katika mpango ujao wa bajeti lakini kwa sasa shule hii itakuwa kama shule dada ya shule ya miembeni mpaka hapo itakapo pata usajili kamili.

Hivyo ametaja wazi kuwa shule hiyo ambayo itakuwa na miundombinu ya kisasa na ujenzi wa choo bora ambacho kitajengwa sambamba na Zahanati ya Lumbanga ambayo itajenga jirani na eneo hilo la shule.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya ya Malinyi ,Marcelin Ndimbwa, akikagua madarasa ambayo yamejengwa kwa ajli ya watoto wa wafugaji Rumbanga.
Mkurugenzi wa malinyi,Marcelin Ndimbwa, akionyesha choo kilichokuwa kikitumiwa na wanafunzi hao.
sehemu ya ubao wa kufundishia wa shule hiyo ya manyasi.
mkurugenzi wa malinyiMarcelin Ndimbwa akitoka darasani katika shule ya msingi Rumbanga.

KURASA ZA MAGAZETI YA TANZANIA IJUMAA JANUARI 6,2017

KIKAO KAZI NGAZI YA MAKATIBU WAKUU CHAFANYIKA ZANZIBAR KUJADILI CHANGAMOTO ZA MUUNGANO

$
0
0
Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais - Zanzibar Bw. Joseph Meza (wa kwanza kulia) akiongoza kikao kazi cha Makatibu Wakuu kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katikati ni Mwenyekiti Mwenza Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Prof. Faustin Kamuzora. Kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Muungano kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Dar es Salaam Bw. Baraka Rajab. Kikao kazi hicho kimefanyika leo tarehe 05/01/2017 katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar na kwa pamoja wamejadili changamoto za Muungano.

Baadhi ya Makatibu Wakuu kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakifuatilia kikao kazi kilichojadili changamoto za Muungano. Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa zamani wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Bw. Shomari Omar Shomari Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji, Bi. Fatma Gharib Bilal Katibu Mkuu Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto na Bi. Khadija Bakari Juma Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya amali kwa pamoja wakifuatilia kikao kazi kilichojadili changamoto za Muungano na namna bora ya kuzipatia ufumbuzi.
Mwenyekiti na Mwenyekiti Mwenza Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais - Zanzibar Bw. Joseph Meza (wa pili kulia) na Prof. Faustin Kamuzora (wa tatu kutoka kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Makatibu Wakuu kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mara baada ya kumalizika kwa kikao kazi.
Pichani ni Mwenyekiti na Mwenyekiti Mwenza Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais - Zanzibar Bw. Joseph Meza (wa pili kulia) na Prof. Faustin Kamuzora (wa tatu kutoka kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Sekretarieti iliyoratibu kikao hicho ikiwa na wajumbe kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

DC AINGILIA KATI MGOGORO WA WAFUGAJI NA MWEKEZAJI WA SHAMBA LA MKONGE MARUNGU MKOANI TANGA

$
0
0
 Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa akizungumza wakati wa mkutano wa wananchi wa Kijiji cha Marungu ambao ni sehemu ya waathirka na mgogoro huo sambamba na muwekezaji wa shamba hilo na kusema kuwa makubaliano yaliyofikiwa baina ya serikali na wafugaji hao lazima yatekelezwe kwa wakati ili kuepusha vurugu za uvunjifu wa amani uliokuwa ukijitokeza mara kwa mara.
 Katibu Tawala wa wilaya ya Tanga(DAS),Faidha Salim akizungumza katika mkutano huo
 Diwani wa Kata ya Marungu (CCM) Mohamed Mambea akizungumza wakati wa mkutano huo
 Mkuu wa wilaya ya Tanga,Thobias Mwilapwa katikati akiandika baadhi ya maswali ya wananchi ambao walikuwa wakiuliza kwenye mkutano huo.
 Wananchi wakifuatilia mkutano wa hadhara wa Mkuu huyo wa wilaya.




MKUU wa Wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa ameingilia kati mgogoro wa wafugaji na mwekezaji wa shamba la mkonge la Marungu Mkoani Tanga na kutoa miezi mitatu kwa wafugaji hao kuhakikisha wanaondoka katika shamba hilo kabla ya serikali haijatumia nguvu ya kuwahamisha.


Akizungumza katika kikao cha wananchi wa Kijiji cha Marungu ambao ni sehemu ya waathirka na mgogoro huo sambamba na muwekezaji wa shamba hilo na kusema kuwa makubaliano yaliyofikiwa baina ya serikali na wafugaji hao lazima yatekelezwe kwa wakati ili kuepusha vurugu za uvunjifu wa amani uliokuwa ukijitokeza mara kwa mara.


Maamuzi hayo yamekuja ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo lililotolewa siku chache zilizopita na Mh;WAziri MKuu la kuwataka Wakuu wote wa Wilaya nchi nzima kuhakikisha wanamaliza migogoro ya ardhi iliyondani ya uwezo wao ili kutoa fursa kwa wananchi kuendelea na shughuli zao.


Mwilapwa alisema kumekuwepo na madhara mengi yanayojiketokeza kutokana na kuwepo kwa migogoro ya wakulima na wafugaji hadi kufikia kutokea mapigano yanayohatarisha amani iliyopo baina ya makundi hayo mawili jambo ambalo serikali imejidhatiti kumaliza migogoro hiyo kwa makubaliano ya mazungumzo.


“Kumekuwepo na mapigano ya mara kwa mara baina ya wakulima,mwekezaji na wafugaji jambo linalovunja amani na hata kuhatarisha maisha ya watu nisema ikiwa makubaliano haya hayatatekelezwa basi Serikali itaingilia kati na itawahamisha wafugaji hao kwa nguvu”Alisema Mwilapa.


Kwa upande wa Diwani wa kata ya Marungu Mohamed Mwambea alisema kuwepo kwa wafugaji hao katika shamba hilo ndani Kijiji hicho kumeleta madhara makubwa kutokana na kutokea mapigano  kwa pande hizo mbili na kutokea uharibifu wa mazao ya wananchi wanaojishughulisha na kilimo Kijijini hapo.


Mwambea alisema imekuwa kawaida kwa wafugaji kushinda katika kesi zao dhidi ya wakulima jambo linaloshangaza wanapata wapi haki ya kuweza kushinda kila aina ya kesi zinazojitokeza baina ya wakulima na wafugaji.


“Ifike wakati kwa Serikali iwe inatenda haki kwa wakulima dhidi ya wafugaji ili kujenga usawa kwa jamii hizo mbili ambazo zinaingia katika migogoro inayohatarisha maisha yao na hata jamii inayotuzunguka”Aalisema Mwambea.


Nae Meneja wa shamba la mkonge la Marungu Casmir Joackim alisema wameshindwa kuendelea na uzalishaji katika shamba hilo kwa zaidi ya miaka miwili kutokana kuingiliwa na wafugaji hao waliohamishia shughuli zao za kifugaji na makazi katika shamba hilo.


Joackim alisema dhamira ya muwekezaji wa shamba hilo ni kutekeleza agizo la Serikali ya awamu ya tano ya kuwataka wawekezaji wote nchini wayaendeleze mashamba yao kiuzalishaji na hata kutoa ajira kwa wananchi ili kukwepa mkono wa Serikali unaoweza kufuta hati ya umili wa shamba hilo na kurudishwa serikalini kwa ajili ya kugawiwa upya wananchi.


“Ikiwa ndani ya shamba letu wapo wafugaji wanaendelea na shughuli zao za ufugaji pamoja na maisha kwa ujumla tangu mwaka 2014 ni namna gani tunaweza kundeleza shughuli zetu,huoni mkono wa Serikali unaweza kutukumba lazima tutendewe haki kwa hawa watu ambao ni wavamizi”Alisema Joackim.

NDEGE ZISIZO NA RUBANI SASA KUBEBA ABIRIA MWAKA 2020

$
0
0

Kampuni moja ya Israel imesema ndege isiyokuwa na rubani, ambayo ilikamilisha safari yake ya kwanza kabisa ikipaa juu ya maeneo tambarare mwezi Novemba, huenda ikaanza kutumika rasmi kufikia 2020.

Ndege hiyo imeundwa na kufanyiwa kazi kwa kipindi cha miaka 15, lengo likiwa kutumika katika juhudi za uokoaji au shughuli za kijeshi.

Ndege hiyo ambayo inafahamika kwa sasa kama Cormorant iligharimu $14m (£11m) na inaweza kubeba mizigo ya uzani wa kilo 500 (1,100lb) na kwenda kwa kasi ya kilomita 185 kwa saa (115mph).

Kampuni ya Urban Aeronautics imesema ndege hiyo ina rafadha (mapanga yanayozunguka kwa kasi ili kuendesha chombo) zilizo ndani na hilo linaifanya kuwa salama zaidi kushinda helikopta.

Kandi na kuweza kupaa juu na kutua bila kuhitajika kusonga mbele au nyuma, inaweza kupaa kupitia kati ya majumba na hata kupitia chini ya nyaya za umeme.

"Hili linafungua njia ya kustawisha Cormorant kutoka kwa hatua ya majiribio hadi uzalishaji kamili karibuni na hatimaye kuanza kutumiwa kibiashara kwa teknolojia hii - kwa shughuli mbalimbali," alisema afisa mkuu mtendaji wa Urban Aeronautics Rafi Yoeli.

Ndege zisizo za rubani zimeanza kupata umaarufu katika kutumiwa kibiashara.

Amazon majuzi walitangaza kuanzishwa kwa huduma ya Prime Air, ambapo ndege zisizo na rubani zinatumiwa kusafirisha bidhaa kwa wateja.

Mwezi Juni, ndege nyingine isiyo na rubani ambayo iliungwa na kampuni ya Ehang kutoka China ilipewa idhini ya kufanyiwa majaribio jimbo la Nevada, Marekani.

Mtaalamu wa ndege zisizo na marubani Ravi Vaidyanathan anasema mafanikio ya safari ya majaribio ya ndege hiyo ya Israel ni ufanisi mkubwa na kwamba ni uamuzi wa busara kwanza kuitumia kwa juhudi za uokoaji na shughuli za kijeshi.


Lakini ingawa huenda muda mfupi baadaye zikatumiwa kwa safari za kiraia - na kusaidia kufika hasa maeneo yasiyo na miundo mbinu au yenye misongamano ya magari - bado ni mapema kujua hilo litatekelezwa kikamilifu linu.

"Kuna changamoto nyingi za kihesheria, mfano kuhusu ni wapi unaruhusiwa kupaa? Ni wapi unaweza kutua? Unaruhusiwa kupaa juu hadi wapi?" alisema.

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII,PROF,JUMANNE MAGHEMBE AZINDUA BODI MPYA TANAPA

$
0
0

Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof,Jumanne Maghembe akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) iliyofanyika katika ukumbi wa Mahakama ya Afrika jijini Arusha.
Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof ,Jumanne Maghembe .
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Mkuu wa Majeshi Mstaafu ,Jenerali George Waitara akifuatilia hotuba ya uzinduzi wa Bodi hiyo iliyotolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii ,Prof,Jumanne Maghembe.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akimkabidhi vitendea kazi Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi ambaye pia ni mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Tanapa .
Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akimkabidhi vitendea kazi Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Tanapa Dkt Chanasa Mpelumbe Ngeleja.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akimkabidhi vitendea kazi Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Tanapa Prof Wineaster Anderson
Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akimkabidhi vitendea kazi Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Tanapa Prof,Alexander Songorwa.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akikabidhi vitendea kazi Devota Mdachi mjumbe wa bodi ya Wadhamini wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) .
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Mkuu wa Majeshi Mstaafu ,Jenerali George Waitara akitoa salam zake wakati wa uzinduzi wa Bodi hiyo uliofanika katika ukumbi wa Mhakama ya Afrika jijini Arusha.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini iliyomaliza muda wake Modestus Lilungulu walpkutana katika hafla fupi ya uzinduzi wa bodi mpya .
Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi ambaye pia ni mjumbe wa Bodi hiyo akifanya utamburisho wa wajumbe wa bodi ya Wadhamini wa shirika hilo.
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA,Prof,Wineaster Anderson ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Taasisi ya Maliasili na Utalii endelevu Afrika (NARESTi Africa) akitamburishwa kwa wafanyakazi wa Shirika hilo.
  Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA, Dkt Lucy Lugwisa kutoka Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira akitamburishwa kwa wafanyakazi wa Shirika hilo.
  Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA,Prof,Alexander Songorwa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Wanyamapori kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii akitamburishwa kwa wafanyakazi wa shirika hilo.
  Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA,Kamishna Marijani Nsato ambaye pia ni Mkuu wa Operesheni na Mafunzo Makao Makuu ya jeshi la Polisi akitamburishwa kwa wafanyakazi wa shirika hilo.
  Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA,Dkt Chanasa Mpalumbe Ngeleja ambaye pia ni Daktari Mkuu wa Mifugo ,Wizara ya Kilimo ,Mifugo na Uvuvi akitamburishwa kwa wafanyakazi wa shirika hilo.
  Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA,George Fumbuka ambaye pia ni Mtendaji Mkuu na Mwenyekiti wa Kampuni ya Core Securities akitamburishwa kwa wafanyakazi wa shirika hilo.
Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya TANAPA,Devota  Mdachi ambaye pia ni Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii nchini akitamburishwa kwa wafanyakazi wa Shirika hilo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) iliyomaliza muda wake ,Modestus Lilungulu akitoa salam zake wakati wa uzinduzi rasmi wa Bodi mpya ya Wadhamini ya TANAPA.
Baadhi ya wafanyakazi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakifuatilia uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Mahakama ya Afrika jijini Arusha.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA),Mkuu wa Majeshi Mstaafu,Jenerali George Waitara (kushoto) akizungumza jambo na Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof ,Jumanne Maghembe mara baada ya kuzinduliwa kwa Bodi hiyo.katikati ni Mkurugenzi wa TANAPA,Allan Kijazi.
 Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) muda mfupi baada ya bodi hiyo kuzinduliwa.
 Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakiwa katika picha ya pamoja na Wakurugenzi wa idara mbalimbali katika shirika hilo.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe pamoja na Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) wakiwa katika picha ya pamoja na mameneja katika shirika hilo. 

Dkt Shein aweka jiwe la msingi Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali iliyopo huko Mazizini, Wilaya ya Mjini, Unguja

$
0
0


Na Rajab Mkasaba, Ikulu
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameweka jiwe la msingi Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali na keleza kuwa bado kuna tatizo la ukusanyaji, utumiaji na uhifadhi wa takwimu hapa nchini hivyo kuna haja ya kuwekwa mfumo madhubuti katika kuondoa hitilafu hiyo. 
Dk. Shein aliyasema hayo, katika hotuba yake aliyoitoa mara baada ya kuweka jiwe la msingi Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali iliyopo huko Mazizini, Wilaya ya Mjini, Unguja ikiwa ni miongoni mwa shamrashamra za miaka 53 ya Mapinduzi ya matukufu ya Zanzibar. 
Katika maelezo yake, Dk. Shein alisema kuwa udhaifu katika utoaji wa takwimu na taarifa, ni ukiukaji wa maadili ya uongozi na utumishi wa ummma kwa msingi huo aliagiza kwa kila Wizara ihakikishe inakuwa na mtaalamu wake wa takwimu katika Idara ya Mipango na Sera, ili kuimarisha utoaji wa takwimu. 
Dk. Shein alisema kuwa taarifa sahihi haziwezi kupatikana bila ya kuwa na mfumo mzuri wa kitaalamu wa ukusanyaji wa takwimu huku akisisitiza kuwa suala la kuwapa wananchi  habari na taarifa sahihi za Serikali ni haki yao ya kikatiba na halina budi kutekelezwa ipasavyo.
“Mimi mwenyewe ni mtumiaji mkubwa wa takwimu, lakini unapohitaji takwimu kutoka Wizarani  basi kwa wakati mmoja tarajia kupata takwimu tofauti’,alisema Dk. Shein. 
Aidha, Dk. Shein alisisitiza kuwa kuna haja ya kuondokana na utaratibu uliopo hivi sasa wa kila mmoja kuwa na mamlaka ya kutoa takwimu za Serikali na kueleza kuwa utoaji wa takwimu muhimu za Serikali una taratibu zake. 
Hivyo, alieleza haja kwa Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa Serikali kutoa miongozo kwa Wizara na Serikali juu ya njia bora za kukusanya, kutoa na kutumia takwimu na nani katika ngazi ya Wizara anaweza kutoa takwimu. 
Pamoja na hayo, Dk. Shein alisisitiza haja kwa hiyo kuhakikisha kuwa inaandaa utaratibu wa kutoa elimu kwa wananchi kuhusu takwimu na umhimu wake kwa jamii, kwenye ngazi mbali mbali.
Pia, alitumia fursa hiyo kuiagiza Wizara ya Fedha na Mipango kuongeza kasi ya kuwasomesha wafanyakazi wanaohusika na takwimu, ili kupatikane wataalamu wa kutosha, watakaoweza kukusanya na kutoa tafsiri mbali mbali za takwimu na uhusiano wake wka maendeleo hapa ya hapa nchini. 
Kutokana na umuhimu wa takwimu Dk. Shein alieleza azma ya Serikali kutoa semina maalum kwa viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa lengo la kuelewa suala zima la takwimu na hatimae kusaidia kufanya kazi kwa haraka na ufanisi zaidi. 
Sambamba na hayoeleza kuwa katika suala zima la kulitafutia soko zao la karafuu, Zanzibar imekuwa ikishindana na nchi nyingi zinazozalisha zao hilo duniani kwenye bei na ubora sambamba na sifa ya karafuu, hivyo Zanzibar ni lazima ijidhatiti katika kuhimili ushindani. 
Dk. Shein alitumia fursa hiyo kuiopongeza Ofisi hiyo kwa ujenzi huo kwa mashirikiano ya pamoja na SMZ, SMT na Benki ya Dunia  nhuku akisisitiza kuwa takwimu ndizo zinazowezesha kujipima na kujitathmini kwani ndio kiii cha nchi. 
Nae Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Khalid Salum Mohammed  alieleza kuwa ujenzi huo ni agizo la Rais Dk. Shein la kutaka kila taasisi ya Serikali iwe na jengo linalokwenda na wakati uliopo huku akieleza azma ya kuzipatia Ofisi za takwimu  ofisi Pemba katika majengo mapya ya Ofisi yanayotarajiwa kuejengwa kisiwani humo. 
Pamoja na hayo, Dk. Khalid alieleza mikakati iliyowekwa na Wizara yake katika utekelezaji wa suala zima la takwimu huku akieleza jinsi Wizara ilivyofanikiwa kuzigundua taasisi zinazovujisha mapato ya serikali na kumuahidi Rais kuwa ataziwasilisha kwake mara tu baada ya kumaliza sherehe za Mapinduzi. 
Nae Naibu Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Ashatu Kijaji alitumia fursa hiyo kueleza kuwa ujenzi huo unakwenda sambamba na ujenzi wa jengo jengine kama hilo la Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania huko Dodoma. 
Dk. Kijaji alitumia nafasi hiyo kumuomba Mkurugenzi Mkaazi wa Benki ya Dunia kuendelea kuzisaidia taasisi hizo za takwimu ili kwa pamoja ziweze kukamilisha miradi yote miwili na kueleza  kuwa takwimu  ndio masikio na macho ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025 kwa Tanzania Bara na 2020 kwa Zanzibar. 
Alitoa pongezi kwa kutekeleza kwa kasi kubwa kauli mbiu ya Serikali ya HAPA KAZI TU!!  Na kuishukuru Benki ya Dunia, Shirika la Maendeleo la Uingereza DFID, Canada na Umoja wa Ulaya kwa kuunga mkono tasinia ya takwimu hapa nchini. 
Nae Mwakilishi wa Benki ya Dunia Elizabeth Ann Talbert alieleza umuhimu wa takwimu katika maendeleo ya nchi huku akiahidi kuwa Benki hiyo itaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuimarisha takwimu. 
Mapema Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Bi Mayasa Mahfoudh Mwinyi alileza kuwa kiini cha ujenzi wa jengo hilo la takwimu ni kuongezeka kwa mahitaji ya takwimu katika sekta za kiuchumi na kijamii. 
Alisema kuwa mahitaji hayo yamepelekea kuongezeka kwa idadi ya wataalamu wa fani ya takwimu sambamba na kuongezeka kwa mahitaji ya vifaa na nafasi za kufanyia kazi ikiwemo mazingira bora ya kazi. 
Bi Mayasa alieleza historia ya kuazishwa kwa Ofisi hiyo pamoja na viongozi walioongoza ambapo alieleza kuwa ujenzi wa jengo hilo umeanza rasmi mwezi Oktoba 2015 na unatarajiwa kukamilika mwezi Aprili mwaka huu ambapo ujenzi huo unakadiriwa kugharimu jumla ya shilingi bilioni 7.9 hadi kukamilika kwake. 
Ujenzi huo umejengwa na Mkandarasi “Messrs World Class Engineering and Contractors Limited” pamoja na Msimamizi wake Y & P Architects (T) Limited zote ni Kampuni za Kizalendo zilizopo Tanzania ambapo jengo hilo litakuwa na ghorofa nne. 

Viongozi mbali mbali walihudhuria hafla hiyo akiwemo Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd, Spika wa Baraza la Wawakilishi na viongozi wengine wa Serikali, Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa Zanzibar, viongozi wa dini na wananchi mbali mbali.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATEMBELEA MGODI WA MAKAA YA MAWE YA NGAKA WILAYA YA MBINGA MKONI RUVUMA

$
0
0


*Aahidi kutuma Gavana, CAG, Msajili wa Hazina kufanya ukaguzi
*Asema Serikali haitaruhusu uagizaji wa makaa hayo kutoka nje ya nchi
*Autaka uongozi wa kampuni uimarishe teknolojia ili kuongeza uzalushaji

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa atamtuma mara moja Msajili wa Hazina aende kufanya uchunguzi wa kina na wa kijinai (forensic investigation) ili kijiridhisha kama mapato na matumizi ya kampuni ya TANCOAL ni halali.

Ametoa kauli hiyo leo mchana (Ijumaa, Januari 6, 2017) mara baada baada ya kupokea taarfa na kutembelea mgodi huo ili kuona shughuli za uzalishaji zikoje.

Waziri Mkuu amesema atamwagiza pia mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ili apitie mahesabu ya kampuni tangu mwaka 2011 walipoanza uzalishaji. “Mbali CAG, itabidi Gavana wa Benki Kuu naye aangalie utumaji wa fedha uliokuwa ukifanywa kama ulifanyika kwa halali,” amesema.

Katika maswali aliyoyauliza Waziri Mkuu, alitaka kujua ni kwa nini kampuni hiyo haijalipa gawio kwa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) ambao ni mbia (asilimia 30) na kampuni ya Intra Energy Limited (asilimia 70) licha ya kuwa imekuwa ikifanya uzalishaji wa makaa ya mawe na kuyasafirisha kwenye viwanda hapa nchini na nje ya nchi.
“Taarifa zenu zinaonyesha kuwa mmepata kila mwaka lakini rekodi nilizonazo zinanionyesha kuwa mwaka 2013 mlipanga kuzalisha tani 50,000 na mkauza zaidi ya hapo. Mkagzi wa hesabu anasema kampuni imepata, hii itawezekanaje?” alisema wakati akimhoji Mkurugenzi Mtendaji wa NDC, Bw. Mlingi Mkucha.
“Desemba 2013 mliuza tani 39,000 kwa wamiliki wa viwanda vya nguo, pia mliuza tani 2,000 kwa kampuni ya saruji ya Zambia, Novemba 2013 mliingia makubaliano ya kuuza tani 165,000 kwa kampuni ya saruji ya Kitanzania na ziliuzwa. Mbona financial statement zenu zinasema mwaka huo nao mlipata hasara?”
“Mnasema gawio (dividend) hutolewa baada ya mtu kutangaza faida. Mbona mlivuka lengo lakini mkatangaza kuwa kamouni imepata hasara katika mwaka huo wa fedha?”
Waziri Mkuu alimbana Bw. Mkucha aeleze ni kwa nini akiwa mwanasheria wa NDC aliruhusu kuwepo kwa mkataba unaotoa mwanya kwa kampuni ya TANCOAL kulipia gharama za menejimenti kwa wakurugenzi ambao wako Australia wakati hawahusiki na utendaji wa kila siku wa TANCOAL hapa nchini.
Pia alihoji ni kwa nini aliyekuwa Mkurugenzi wa NDC, Bw. Gideon Nassari alikuwa ni mjumbe wa Bodi ya TANCOAL na mjumbe wa Bodi ya Intra Energy Corporation ya Australia huku akiwa ni Mtendaji Mkuu wa NDC. “Wewe ulikuwa mwanasheria wa NDC na ulilijua hilo lakini hukuona taabu ya kiutendaji katika hilo? Au ulishindwa kusema kwa sababu alikuwa ni bosi wako?”
Waziri Mkuu amemtaka Bw. Mkucha aupeleke mikataba huo kwa MwanasheriA Mkuu wa Serikali ili aupitie upya na hasa kipendgele cha kufungua akaunti za NDC kwa kutumia kanuni za Australia na suala la utaratibu wa gawio kwa wanahisa ambapo kifungu kilichopo kinaipa Bodi ya TANCOAL mamlaka ya kuamua kutoa au kutokutoa kwa wanahisa.

“Kipengele kama hiki kwenye mikataba kinazuia ninyi kupata gawio, na ndiyo maana hesabu zao kila mwaka zimekuwa zinasoma hasara na ninyi mnaona sawa tu huku Serikali ikiendelea kukosa mapato yake,” amesema.

Waziri Mkuu ameutaka uongozi wa kampuni ya TANCOAL uongeze uzalishaji ili iweze kukidhi mahitaji ya ndani kwani makampuni mengi yamebaini gharama kubwa iliyopo kwenye matumizi ya mafuta ya dizeli na sasa yanahitaji makaa ya mawe kwa uzalishaji.
“Nimetembelea mgodi na kujiridhisha kuwa makaa ya mawe yapo ya kutosha. Uongozi wa kampuni mmesema mashine ziko bandarini Mtwara, lipieni mkamilishe taratibu ili mashine na mitambo yenu vije kusaidia kuongeza uzalishaji,” amesema.
“Nirudie wito wa Serikali kuwa hatutaruhusu uagizaji wa makaa ya mawe kutoka nje ya nchi na kwa maana nyingine tumewaongezea wigo wa soko lakini ninyi mnakosa teknolojia ya uchimbaji makaa kwa wingi. Fanyeni haraka kuleta hivyo vifaa vilivyoko bandarini,” alisisitiza.
Akiwa kwenye mgodi huo, Waziri Mkuu alielezwa kuwa kampuni hiyo imepanga kuongeza uzalishaji na kufikia tani 60,000 kutoka tani 2,500 za sasa. Hivi sasa, uchimbaji kwenye mgodi wa Ngaka unafanyika kwenye eneo la Mbalawala na Mbuyura ambayo yana mashapo (deposits) ya tani milioni 423.
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU
IJUMAA, JANUARI 6, 2017.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya Tancoul Bwana Mark McAnderew  wakati alipotembelea mgodi wa makaa ya mawe ya Ngaka unaomilikiwa na kampuni ya Tancoul uliopo wilayani Mbinga  kushoto kwa waziri mkuu ni Mwenyekiti wa bodi ya NDC Dr Samuel Nyantahe
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na mkurugenzi mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Mlingi Mkucha wakati alipotembelea mgodi wa makaa ya mawe wa Ngaka unaomilikiwa na kampuni ya Tancoul uliopo wilayani Mbinga  kushoto kwa waziri mkuu ni Mwenyekiti wa bodi ya NDC Dr Samuel Nyantahe
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Ofisa Rasilimali watu wa kampuni ya Tancoul Ms  Pendo Mweli wakati alipotembelea mgodi wa makaa ya mawe unaomilikiwa na kampuni ya Tancoul uliopo Ngaka wilayani Mbinga  Mkoani Ruvuma
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia shughuli za uchimbaji wa makaa ya mawe unavyofanywa nakampuni ya Tancoul katika mgodi wa Ngaka uliopo wilayani Mbinga  kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la maendeleo la taifa NDC Dr Samuel Nyantahe.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia mkaa wa mawe ulivyo
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa ameongozana na mkuu wa mkoa wa Ruvama Mhandisi Mahenge pamoja naviongozi mbalimbali walipokuwa wanatemmbelea mgodi wa Ngaka

Picha na Chris Mfinanga

Wakuu wa wilaya za Arusha wabebeshwa mzigo mzito.

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo(kwanza kulia) akizungumza katika kikao cha maandalizi ya Bajeti 2017/2017 na mapitio ya Bajeti 2015/2016.
Na Nteghenjwa Hossea, Arusha
Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Arusha wameagizwa kusimamia Halmashauri zao kujibu hoja zote zilizowasilishwa na  Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa  Hesabu za Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016 kabla ya kufika mwisho wa juma lijalo.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo  wakati wa Kikao  cha maandalizi ya Bajeti ya mwaka 2017/2018 na mapitio ya bajeti ya nusu mwaka wa Fedha 2016/2017 kilichohusisha Halmashauri zote za Mkoa wa Arusha  na wataalam toka Ofisi ya Mkaguzi wa hesabu za Serikali.
Akitoa Agizo hilo Mhe. Gambo alisema “Nataka kila Halmashauri ikamilishe ujibuji wa Hoja kwa wakati na kwa majibu sahihi sio kufanya majibu ambayo yanaibua hoja zaidi au hayajitoshelezi na kwa Halmashauri ambayo ilipata Hati Chafu au Hati ya Mashaka kwa mwaka uliopita ianishe wataalamu waliopelekea Halmashauri kupata Hati hizo ili waweze kuchukuliwa hatua Stahiki”.
Wakuu wa Wilaya mshiriki Kikamilifu kuhakikisha hoja zinajibiwa ipasavyo na wale waliosababisha hoja hizo kwa kipindi cha nyuma wanachukuliwa hatua ili kuleta nidhamu ili kuongeza umakini katika zoezi zima la ujibuji wa Hoja alisema Gambo.
Aliongeza kuwa “Sitamueleza Mkuu wa Wilaya ambaye Halmashauri yake itapata Hati Chafu au ya Mashaka kwa hesabu za mwaka ulioisha, Mkasimamie Halmashauri zenu kwa nguvu zenu zote na katika hili sitamuonea mtu haya”.
Katika mapitio ya Bajeti ya inayoendelea alizitaka Halmashauri ambazo hazijatoa asilimia kumi ya mapato yao kama mikopo kwa vikundi vya wananwake na vijana zikatoe Fedha hizo kabla ya mwisho wa Januari ili kuweza kuinua uchumi wa makundi haya yaliyoainishwa kwa mujibu wa Sera na Maelekezo.
“Katika hili napenda kuwapongeza Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa kukamilisha utoaji wa mikopo  zaidi ya Mil 600 kwa robo ya kwanza naya Pili kwa mwaka wa Fedha 2016/2017 lakini halmashauri zingine zote hazijakamilisha utoaji wa Mikopo inayotakiwa kwa kipindi cha nusu mwaka.”
Awali katika Kikao hicho akiwasilisha mapitio ya Bajeti 2015/2016 na Mpango wa Bajeti 2016/2017 Katibu Tawala Msaidizi huduma za Mipango Bi. Grace Mbaruku alisema Halmashauri zote zinatakiwa kuandaa Bajeti Mpya kwa kuzingatia vipaumbele vilivyowekwa katika muongozo wa Bajeti.
 Halmashauri haitazingatia vigezo vilivyowekwa inaweza kupelekea bajeti yao kukwama katika ngazi za juu hivyo zingatieni vigezo kama kutenga Fedha za Lishe kwa ajili ya kutokomeza udumavu kwa Watoto alisema Bi. Mbaruku.
Akiwasilisha Taarifa ya Changamoto zinaowakabili katika Usimamizi wa Halmashauri Katibu Tawala Msaidizi anayesimamia Serikali za Mitaa Bi. Susane Mnafe aliainisha ucheleweshaji wa uwasilishaji wa Taarifa toka Halmashauri mara zinapohitajika, kutofuata mfumo elekezi wa uwasilishaji wa Taarifa.
Aliongeza kuwa kutokua na kanzidata ya vyanzo vya mapato na uandaaji wa Bajeti ya Halmashauri kabla ya Sheria ndogo mpya kupitishwa huchangia kukwamisha ukusanyaji wa mapato kwa kutumia viwango vipya.

KURASA ZA MAGAZETI YA TANZANIA NA UINGEREZA JANUARI 7,2017

AZAM WAMKARIBISHA LWANDAMINA, WAMPA KIPIGO CHA 4-0

$
0
0
 Amisi Tambwe akipambana na beki wa Azam Yahaya Mohamed  wakati wa mchezo wa hatua ya makundi wa kombe la Mapinduzi uliomalizika kwa Azam kutoka na ushindi wa goli 4-0.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Timu ya Azam Fc imefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali kwa kuipa kipigo cha mbwa mwizi cha bao 4-0  timu ya Yanga huku wakikalia usukani mwa kundi B katika kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar usiku huu.

Mpira ulianza kwa kasi ikionekana Azam FC wamepania kupata bao la mapema Dakika ya kwanza ya mchezo na katika dakika ya 2 Azam wanapata bao kupitia kwa mfungaji wao John Bocco baada ya  kutokuwa na maelewano baina ya mabeki wa Yanga kwenye kuuokoa mpira uliookolewa na golikipa wa Yanga, Deogratius Munish "Dida".


Katika dakika ya 9 Yanga wanafanya shambulizi langoni mwa Azam lakini Saimon Msuva anashindwa kumalizia kazi nzuri iliyofanywa na mrundi Amisi Tambwe.


Baada ya kuonekana kutokuwa na maelewano katika safu ya ushambuliaji Kocha George Lwandamina anafanya mabadiliko kwa kumtoa  Juma Mahadhi na nafasi yake inachukuliwa na Emmanuel Martin katika dakika ya 36. Mpaka Mapumziko Azam 1 Yanga 0.



Kipindi cha pili kinaanza kwa kila mmoja kumsoma mwenzake lakini katika dakika ya 54, Yahaya Mohamed  anaipatia Azam goli la pili baada ya kuunganisha krosi safi Abubakar Salum " Sure Boy".


Wakiwa bado hawaamini Dk 81, Joseph Mahundi anaiandikia Azam goli la tatu baada ya kuachia shuti kali nje ya 18 na kuacha mashabiki wa Yanga wakiduwaa wakiwa hawaamini wanachokiona.


Dk 84, Atta aliyeingia kipindi cha pili anaifungia timu yake bao safi akiunganisha  pasi ya Afful baada ya Mwashiuya kuukosa mpira, na mpaka mpira unamalizika Azam wanatoka kifua mbele wakiwa na alama 7 wakifuatiwa na Yanga wenye alama 6.  


Timu hizi zinasubiri washindi wa mechi za kesho kwenye kundi A ili kupambana nazo kwenye hatua ya nusu fainali.
Kikosi cha Yanga kilichopambana usiku huu.


Kikosi cha Azam kilichopambana usiku huu.
 Wachezaji wakiwa wanafanya mazoezi kabla ya mechi.
 Timu zikiingia uwanjani wakati wa mchezo wa hatua ya makundi kati ya Yanga na Azam 
 Saimon Msuva akimtoka beki wa Azam wakati wa mchezo wa hatua ya makundi wa kombe la Mpoinduzi uliomalizika kwa Azam kutoka na ushindi wa goli 4-0.
 Juma Mahadhi akipambana katikati ya mabeki wa Azam wakati wa mchezo wa hatua ya makundi wa kombe la Mpoinduzi uliomalizika kwa Azam kutoka na ushindi wa goli 4-0.
Frank Domayo (kushoto) akipambana na kiungo wa Yanga Haruna Niyonzima wakati wa mchezo wa Azam na Yanga uliomalizika kwa Azam kushinda 4-0. 
 Wachezaji wa Azam wakishangilian moja ya goli lilofungwa katika mchezo huo leo usiku.
Kiungo wa Yanga Justine Zulu akiwa amebebwa na golikipa wa Yanga Ally Mustafa 'Batez' baada ya kuumia wakati wa mchezo huo na kutolewa nje.

Huawei offers Tsh. 65m/- to boost SUZA TV

$
0
0

 HUAWEI Technologies Co. Ltd offered the fund support to the State University of Zanzibar (SUZA) so as to help the operation of “remote TV-learning” programmes which aim to foster digital education material training and knowledge transfer for middle school students being part of their “Seeds for the Future” programme in Zanzibar. 
The handing over ceremony of US $ 30,000 took place at Tunguu campus on Wednesday 4th January, 2017 in which His Excellency Mr. Xie Xiuouwu, the People’s Republic of China Consul General in Zanzibar on behalf of HUAWEI Technologies Co. Ltd handed over a cheque of the said amount.

The event was also witnessed by Honourable Riziki Pembe Juma, the Zanzibar Minister of Education and Vocational Training who in her welcome speech to H.E. Mr. Xiuouwu informed that the government of Zanzibar is very much thankful for a number of notable contributions in many sectors offered by the government of the People’s Republic of China to Zanzibar. 
“China has been a good friend and partner of Zanzibar since a long time ago, you cannot talk of Zanzibar’s development without mentioning China,” she said. “We welcome HUAWEI to share its global ICT experience to us, give their advice and participate in Zanzibar ICT innovation,” Hon. Riziki continued to say. 
She requested HUAWEI to continue donating more for the benefit of the people of Zanzibar especially in the area of ICT services and informed that the State University of Zanzibar is soon hoping to establish its new School of Computing, Communication and Media; she appealed to HUAWEI also to think of supporting the establishment of this school. 
In his remarks, His Excellency Mr. Xie Xiuouwu stated HUAWEI believes that access to education is vital to create opportunities that support fair and sustainable development in the country,therefore, their corporate social responsibility initiatives largely focus on education and knowledge transfer that is why HUAWEI has been connecting the whole part of Tanzania including Zanzibar with innovative information and communication technologies for over 16 years and will continue to do so.
Through the joint efforts between HUAWEI and the Revolutionary Government of Zanzibar, the Government of the United Republic of Tanzania, and local partners, we are glad to see that more than 70% of country’s population is being connected by HUAWEI’s ICT technologies and enjoy the convenience of a digital world,” he explained. 
He added that the decision of HUAWEI to support SUZA on its remote TV –Learning project which will definitely leverage the teachers shortage and solve or minimize the problem of teaching and learning material shortage situation for most of schools in Zanzibar. “We believe that SUZA“remote TV-learning program” will help a lot on improving education level in middle schools in Zanzibar,” he noted. 
Responding to Hon. Riziki’s request, Mr. Xiuouwu informed that as a long-term investor and responsible citizen in Zanzibar, HUAWEI wishes to see a well- developed Zanzibar and that to realize this goal they will continue to bring in more innovative ICT technologiesto digitalize Revolutionary Government of Zanzibar in different disciplines. “I believe that with our joint efforts, innovation will transform Zanzibar to a prosperous digital society,” he said. 
Prof. Idris Rai, the SUZA Vice Chancellor, while giving his welcome remarks showed his appreciation by saying that SUZA appraises the support offered by HUAWEI pointing out this will largely boost up the production of intended educational programmes hence benefit the stakeholders at large. He urged the donors to continue offering their contributions to the station so as to enliven it.

Timu ya kuchunguza chanzo cha moto soko kuu la Kayanga yaundwa

$
0
0

 Na Mwandishi wetu.
Kufuatia kuungua kwa mara ya pili kwa soko kuu la kayanga katika Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe, Ofisi ya Mkuu wa mkoa Kagera imeiagiza Halmashauri hiyo kuunda timu mara moja na kuanza uchunguzi wa chanzo cha moto huo katika soko hilo, ambalo kwa mara ya kwanza liliungua  tarehe 11 Machi, 2016.

Sehemu ya soko kuu la Kayanga imeungua usiku wa kuamkia tarehe 7 Januari, 2017, saa 9:00 usiku, ambapo vibanda 52 vilivyojengwa kwa mbao na meza 24 za wafanyabashara wadogowadogo wa nafaka, matunda na mbogamboga vimeteketea kwa moto pamoja na mali za wamachinga waliokuwa wanapanga chini wapatao 33 nao mali zao zimeteketea kwa moto.

Akiongea mara baada  ya kukagua athari za janga la moto katika soko hilo Katibu tawala wa Mkoa wa Kagera Kamishina Diwani Athumani, leo tarehe 7 Januari, 2017,  na kuteketeza sehemu ya soko kuu la Kayanga wilayani Karagwe kwa mara ya pili ikiwa limewahi kuungua, amebainisha kuwa tayari Halmashauri ya wilaya hiyo imeshatekeleza maelekezo yao ya kuunda timu ya uchunguzi ambayo inaanza kutekeleza majukumu yake kesho, tarehe 8 Januari, kwa muda wa siku nne.

“Tumeunda timu tujue kwa nini hili soko linakuwa na majanga ya moto ya mara kwa mara, nawaomba wananchi wote wa Kayanga toweni ushirikiano wa kutosha kwa timu hii na yeyote mwenye taarifa ya chanzo cha moto awasilishe taarifa zake kwenye kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hii”  Alisisitiza Athumani.
Aidha, Athumani alifafanua kuwa yeyeyote atakaye bainika kuwa ndo chanzo cha kusababisha majanaga ya moto kutokea mara kwa mara katika soko  hilo hatua stahiki zitachukuliwa kwa kuwa  kuungua kwa soko hilo kumekuwa kusababisha hasara kubwa kwa wafanyabiara wa soko hilo.
Akiongea wakati wa ziara hiyo, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Adeodata  Agustine, amefafanua kuwa thamani ya awali ya mali iliyoteketea inakisiwa kuwa Tsh, 80,000,000/= (mazao ya nafaka, mbogamboga , matunda pamoja na nguo na bidhaa za dukani), na thamani ya vibanda ni Tsh, 52,000,000/= na meza ni 9,600, 000/=.

“Chanzo cha moto hadi sasa hakijajulikana na kikosi cha zimamoto kwa kushirikiana na na Polisi na TANESCO wanaendelea na uchunguzi, taarifa hii ni ya awali tutapata taarifa kamili ya thamani ya mali na chanzo cha  janga la moto baada ya timu kukamilisha kazi kwa muda uliopangwa” alisema Adeodata.

Naye mwenyekiti wa Wafanyabiashara wa Soko kuu la Kayanga, Wilton William, aliishukuru halmashauri hiyo kwa juhudi walizo zifanya za kuzima moto huo pamoja na hatua walizozichukua za kuchunguza chanzo cha moto huo amabao umeunguza soko hilo kwa mara ya pili mfululizo.

Soko la Kayanga lina jumla ya vibanda 257, ambapo  vibanda 122  vimejengwa kwa matofari, na vibanda 135 vimejengwa kwa mbaao.  Katika tukio la janaga la moto la mwaka jana vibanda 117 ikiwa  ni viband 83 vya mbaao na 34 vya tofari viliteketea kwa moto.
 Katibu tawala Mkoa wa Kagera Kamishina, Diwani Athumani akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe, Adeodata Agustine juu ya janga la moto katika soko kuu la Kayanga alipotembelea soko hilo kujionea athari za moto tarehe 7 Januari 2017.
Katibu tawala Mkoa wa Kagera Kamishina, Diwani Athumani (katikati) akipata maelezo ya uratibu wa majanga kutoka kwa  Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu, Brg. Jen. Mbazi Msuya wakati alipotembelea soko hilo kujionea athari za moto tarehe 7 Januari 2017 (kushoto) ni Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe, Adeodata Agustine.(PICHA ZOTE NA OFFISI YA WAZIRI MKUU)
 Baadhi ya Wafanyabiashara wa mazao ya nafaka wakipakia mabaki ya mazao  yao baada ya vibanda vyao vya biashara kuungua moto kufuatia moto uliozuka usiku wa saa 9:00 usiku wa tarehe 7Januari, 2017,  na kuteketeza sehemu ya soko kuu la Kayanga wilayani Karagwe kwa mara ya pili ikiwa limewahi kuungua tarehe 11 Machi 2016.
 Muuonekano wa Soko Kuu la Kayanga  baada ya vibanda  vya baadhi ya wafanyabiashara kuungua moto kufuatia moto uliozuka usiku wa saa 9:00 usiku wa tarehe 7 Januari, 2017, ikiwa soko hilo limewahi kuungua tarehe 11 Machi 2016.

MAGAZETI YA TANZANIA JUMAPILI JANUARI 8,2017


ALIYEWAUA WATU 5 MAREKANI AKAMATWA

$
0
0
Share this Post
Mshukiwa alikuwa mwanachama wa kikosi cha ulinzi cha Puerto Rico na AlaskaPolisi katika jimbo la Florida wanamzuilia mwuaji mshukiwa baada ya watu watano kupigwa risasi na kuawa na wengine wanane kujeruhiwa katika uwanja wa ndege wa Lauderdale.Shambulizi hilo lilitokea katika eneo la kupokea mizigo. Lengo la shambulizi hilo halijulikani.
Mshukiwa ametajwa kama Estaban Santago aliyepatikana na kitambulisho cha kijeshi na ambaye amewahi kufanya kazi Iraq.Maafisa wa FBI katika afisi ya Alaska wamekuwa na hali ya wasiwasi kumhusu kwa sababu ya tabia zake za zisizoeleweka na mnamo Novemba walimwelekeza kwa daktari bingwa wa akili.Polisi wanasema mshukiwa huyo hakusema lo lote kabla ya mashambulizi au baadaye. Alipoishiwa na risasi alilala chine kwa upole.
Mshukiwa alikamatwa akiwa bila silaha
Watu wakitumia magari kujikinga

Rais mpya Ghana aapishwa, viongozi waliohudhuria sherehe hiyo kujadiliana namna ya kumchomoa Rais wa Gambia aliegomea madarakani

$
0
0
Rais mpya wa Ghana ambaye aliwahi kuwa wakili wa haki za kibinaadamu hapo zamani, Nana Akufo-Addo, ameapishwa rasmi leo kuwa kuwa rais mpya wa nchi hiyo, katika sherehe iliyofanyika katika uwanja wa Independence Square Jijini Accra, Ghana na kuhudhuriwa na viongozi kadha wa Afrika.Katika hotuba yake ya kwanza, Nana Akufo-Addo, alimsifu rais aliyemaliza muda wake madarakani, John Dramani Mahama, kwa namna alivyokiri kushindwa katika uchaguzi wa mwezi uliopita.Viongozi zaidi ya 14 kutoka nchi za Afrika walikusanyika katika mji mkuu wa Ghana, Accra, kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa rais huyo mpya, Nana Akufo Addo.
Rais Akufo Addo, alimshinda Rais John Dramani Mahama, katika uchaguzi wa mwezi uliopita.
Baada ya kuapishwa kwa rais, sasa viongozi waliohudhuria sherehe hiyo, watajadili namna ya kuhakikisha kuwa Rais wa Gambia, Yahya Jammeh, anaondoka madarakani.
Kiongozi huyo amekataa kustaafu ingawa alishindwa katika uchaguzi wa Mwezi Disemba.

MKOA WA ARUSHA KUKOMESHA MIGOGORO YA ARDHI

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo akizungumza kwenye kikao cha kutatua migogoro ya Ardhi mkoani humo.


KARIMJEE JIVANJEE FOUNDATION REWARDS YOUNG SCIENTISTS 2016

$
0
0

Diana Sosoka and Nadhra Mresa (All photos: Daniel Mbega of MaendeleoVijijini Blog)

Diana and her father, Sosoka Paul
Young Scientists Tanzania (YST) Executive Director, Dr Gozbert Kamugisha
 Dr Kamugisha with scholarships
Diana Sosoka, Nadhra Mresa and their teacher Mr Rashid Namila.

By Daniel Mbega of MaendeleoVijijini Blog
Dar es Salaam:THE Karimjee Jivanjee Foundation (KJF) has rewarded Diana Sosoka and Nadhra Mresa from Mtwara Girls Secondary School for being overall winners of the Young Scientists Tanzania (YST) Awards in 2016.
Speaking at a press event to send off the winners to Dublin, Ireland, the KJF Team said the winners would receive scholarship from the foundation to study at any local university when they complete their high school education.
They both take a combination of Chemistry, Biology and Geography and aspire to be medical doctors.
The students are travelling to Dublin today to attend the BT Young Scientists and Technology Exhibition, an Irish annual school students’ science competition, which aims at encouraging interest in science in primary, and secondary schools.
Speaking at the event, the students thanked their school teacher, Mr. Rashid Namila their Biology teacher, whom they said has been a fundamental to their success.
They also thanked the YST, led by Dr. Gozbrt Kamugisha, and the KJF for making their dreams come true.
“Our innovation was based on a locally made incubator to help the women around our school to raise chicken after seeing them come to our school every day to seek for leftovers sue to the poverty situation that has engulfed them,” they said, adding that their technology has inspired various people around Mtwara and across the country to go and learn.
Ms. Eliavera Timoth, the Foundation’s Deputy Marketing Manager, speaking on behalf of KJF Manager Ms. Devota Rubama, said KJF was a non-governmental organization that was registered in 2009 and commenced its operation in 2010 with commitment to support the Tanzanian community, specifically improving education sector.
“The education sector is the core charity notably by providing scholarships to young Tanzanians to be able to accomplish their studies at university level,” she was quoted as saying, adding that the scholarships were provided to students under the category of science in an effort to join hands with to government initiatives, targeting on encouraging students to pursue science subjects.
“We are eager to ecourage and support Tanzania young students to be able to develop various innovative skills through science for the betterment of the nation,” she said.
Speaking of the YST scholarships, Ms. Eliavera said since 2012 the Foundation has provided 17 scholarships to students in the categories of overall winners and winners in special school in need.
“Every year KJF provide 4 schholarships to winner of YST awards to study at university level. We have already provided scholarships to students from Kibosho Secondary School (2012 – 3 scholarships overall winners); Ilongelo Secondary School of Singida (2013 – 2 overall winners scholarships); and Fidel Castro –Pemba (2013 – 2 special school in need scholarships),” Ms. Eliavera said.
Other scholarships were Lumumba Secondary School – Zanzibar (2014 – 2 overall winners); Ngongo Secondary School – Lindi (2014 – 2 special school in need scholarships); Mzumbe Secondary School – Morogoro (2015 – 2 overall winners); Nasa Secondary School – Simiyu (2015 – 2 special school in need); Mtwara Girls (2016 – 2 overall winners); and Binza Secondary School – Simiyu (2016 – 2 special school in need scholarships).
However, Ms. Eliavera said, KJF is planning to launch a dual Masters’ degree in African Cinservation at the University of Glasgow, Scotland and Nelson Mandela University – Afican Institution of Science and Technology in Arusha.
The programme, according to her, is for two years and KJF will provide three scholarships for students to study two terms at Glasgow University and eight terms at Nelson Mandela University.
“The Foundation has been giving scholarships to Doctors to graduate for a Masters’ degree programme in Paediatric Oncology at Muhimbili University of Health and Alllied Sciences (Muhas), two doctors graduated in 2015 and one in 2016,” Ms. Eliavera said.
The Honorary Chairman of Karimjee Jivanjee Group of Companies in Tanzania, Hatim Karimjee said: “We are very honoured to support the Young Scientists Tanzania Award because we believe that education is very important to the future development of Tanzania, and also because science education in particular can open opportunities for higher level career development.”
KJF is the primary vehicle for the Karimjee family’s charitable work.
The mission of the Foundation is to invest in education as a means to enhance the economic development of Tanzania.
At present, many young Tanzanians continue to benefit from scholarships from KJF, which enable them to follow their dreams and to make a greater contribution to Tanzania as a result of their education.
In addition to these scholarships, the Foundation also supports Read International and others; works with Wonder Workshop and is working to boost the capacity for management of pediatric oncology in Tanzania.
Hatim Karimjee said, although KJF’s main focus at the moment is funding educational institutions to improve education capacity, the Karimjee family established several charitable trusts in the 1950’s before independence.
“We have built many schools, hospitals, dispensaries, mosques and community centres. The most famous of our donations is the Karimjee Hall. We built and donated this building to the Dar es Salaam Municipal Council in 1957 as a Town Hall. It was later adapted to become the official seat of Parliament. Independence was declared in Karimjee Hall on 9th December 1961,” he said.
Other important donations by the Karimjee family have been the Usagara Secondary School in Tanga (Formerly Karimjee Secondary School), the Karimjee Clin in Mnazi Mmoja – Dar es Salaam, the old Karimjee Hospital in Zanzibar and the recent donation of 100 desks to Mkwakwani Secondary School in Tanga, a donation that was made to support the Government’s effort to offset the existing countrywide shortage of desks in primary and secondary schools.
The Karimjee Jivanjee Foundation is funded by donations from Toyota Tanzania, one of Tanzania’s biggest and compliant taxpayers, which is celebrating its 50thanniversary as the sole and authorized Toyota distributor in Tanzania since 1965.
(Prepared by www.maendeleovijijini.blogspot.com)

MVUA YAWAATHIRI WANANCHI WILAYANI RUNGWE MKOANI MBEYA

$
0
0

 Mkazi wa Kijiji cha Ndubi kilichopo wilayani Rungwe mkoani Mbeya, Julius Mwambola (kulia), akionyesha migomba iliyoangushwa kutokana na mvua iliyonyesha wilayani humo mwishoni mwa wiki. Kulia kwake ni mke wake Nabwike Swebe.

 Migomba ikiwa imeanguka kutokana na mvua hizo.

 Mwanahabari Dotto Mwaibale, akichukua taarifa ya athari ya mvua hiyo kutoka kwa mkazi wa Kijiji cha Ndubi, Ambokile Mwangosi.

 Nyumba ya Kikongwe, Gwanaloli Ndapapa ikiwa imeezuliwa paa na mvua hiyo ya upepo.
Kikongwe Maria Kamendu (85), akiwa ameshika paa la  nyumba ya jirani yake Gwanaloli Ndapapa iliyobomolewa na mvua iliyonyesha mwishoni mwa wiki katika Kijiji cha Ndubi wilayani Rungwe mkoani Mbeya na kuharibu migomba na baadhi ya nyumba.

Dotto Mwaibale, Mbeya

WAKAZI wa Vijiji vya Ndubi, Mpuguso Kata ya Kisondela Tarafa ya Pakati wilayani Rungwe mkoani Mbeya wameathiriwa na mvua kubwa iliyoambatana na upepo ambayo imeezua baadhi ya mapaa ya nyumba na kuangusha migomba.

Akizungumza kuhusu tukio hilo mkazi wa Kijiji cha Ndubi, Ambokile Mwangosi alisema wamepata pigo kubwa kutokana na mvua hiyo iliyonyesha mwishoni mwa wiki kutokana na migomba mingi kuanguka hivyo kutishia tishio la njaa.

"Siwezi kuelezea kwa undani tathmini ya athari ya mvua hii lakini tumepata pigo kwani kaya nyingi migomba imeangushwa na mvua hiyo" alisema Mwangosi.

Mkazi mwingine wa kijiji hicho Julius Mwambola alisema mvua hiyo imeangusha migomba yake 100 yenye thamani ya sh.250,000.

"Tumeathiriwa kwa kiasi kikubwa na mvua hii kwani mimi binafsi migomba iliyoangushwa na upepo wa mvua hiyo ni zaidi ya 100" alisema Mwambola.

Mkazi mwingine wa Kijiji cha Mpuguso kitongoji cha Nkuju, Tulinagwe Naswila alisema mvua hiyo imeangusha migomba yake 40 yenye thamani ya sh.200,000.

Alisema mvua hiyo ilianza kunyesha saa saba mchana na ilidumu kwa muda wa saa moja na kuleta athari kubwa ya kubomoa baadhi ya nyumba na kuharibu migomba.

"Mvua ilikuwa kubwa ambayoiliharibu migomba na kuezua paa za nyumba kadhaa na kubomoa nyumba ya mjane mmoja aliyemtaja kwa jina la Gwanaloli Ndapapa (85).

Jitihada za kumpata Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Julius Chalya ili kuzungumzia suala hilo zilishindikana baada ya kupigiwa simu mara kadhaa bila ya kupokelewa.

Viewing all 7753 articles
Browse latest View live


<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>